Wakala wa barabara Mjini na Vijijini (TARURA) wilayani Ngorongoro inaendelea kutekeleza ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 46 katika kata ya Oldonyosambu kijiji cha Jema ambalo linatarajiwa kuunganisha kijiji cha jema na vijiji jirani vilivyo katika kata ya Oldonyosambu
Daraja hilo litagharimu kiasi cha shilingi milioni 290 mpaka kukamilika, aidha, daraja hilo linategenewa kutumiwa na Wakazi wa Oldonyosambu na maeneo ya jirani na na kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro amefika na kukagua mradi huo wa daraja licha ya kuridhishwa na maendeleo ya hatua za ujenzi wake ametoa rai kwa TARURA kuhakikisha mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Novemba 2024 daraja hilo liwe limekamilika.
Aidha, Mhe. Sakulo ametumia nafasi hiyo kuzungumza na Wananchi wa kata hiyo na kuwataka kuwa walinzi wa mali za umma na kuhakikisha kila mmoja kwa umoja wao wanakua walinzi wa miradi yote inayotekelezwa na Serikali pamoja na wahisani. Pia, ametoa rai kwa wananchi kulitumia vyema daraja hilo pindi litakapokamilika.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.