• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhamira
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Utumishi
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji na Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba za Vikao
    • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Kata
      • Loliondo
        • Ololosokwan
        • Soitsambu
        • Enguserosambu
        • Maalon
        • Oloirien Magaiduru
        • Piyaya
        • Orgosorok
        • Oloipir
        • Arash
      • Ngorongoro
        • Alailelai
        • Naiyobi
        • Olbalbal
        • Nainokanoka
        • Kakesio
        • Ngorongoro
        • Eyasi
        • Endulen
        • Ngoile
        • Alaitolei
        • Misigyo
      • Sale
        • Sale
        • Malambo
        • Digodigo
        • Oldonyosambu
        • Samunge
        • Pinyinyi
        • Kirangi
        • Engaresero
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezw
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA NGORONGORO AWATAKA VIONGOZI WA TASAF KUONDOA MALALAMIKO YA WANUFAIKA.

Posted on: February 19th, 2025

Ngorongoro, 19 Februari 2025 – Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Multallah Sadiki Mbillu, amewataka viongozi wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF) kuondoa malalamiko ya wanufaika kuhusu malipo yao kwa kuhakikisha mfumo wa manunuzi serikalini (NeST) unatumika ipasavyo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa NeST kwa watendaji wa vijiji na CMC leo, Mbillu alisema amekuwa akipokea malalamiko ya wanufaika wa TASAF wakidai kutopata malipo yao baada ya kufanya kazi. Aidha, baadhi ya malalamiko yamedai kuwa mratibu wa TASAF anahusika na upotevu wa fedha za wanufaika, madai ambayo ameyakanusha na kusisitiza kuwa uwazi na matumizi sahihi ya mfumo wa NeST yatasaidia kuondoa changamoto hizo.

Kwa upande wake, Mratibu wa TASAF Wilaya ya Ngorongoro, Bw. Thomas Nade, alieleza kuwa wanufaika wa ajira za muda chini ya miradi ya TASAF watafanya kazi kwa mikono kwa muda wa masaa manne kwa siku kumi ndani ya mwezi na kulipwa kiasi cha Tsh 30,000, ambapo kila siku watapata Tsh 3,000. Aliwataka watendaji wa vijiji kufanya kazi kwa kujitolea ili kusaidia kaya maskini badala ya kutanguliza maslahi binafsi.

Kuhusu utekelezaji wa miradi ya TASAF kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Bw. Nade alisema wilaya ya Ngorongoro imepokea Tsh 904,743,147.5 ambazo zinatumika kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika Shule ya Msingi Wasso, malambo, bweni katika Shule ya Sekondari Digodigo, jengo la OPD katika Zahanati ya Soitsambu, pamoja na nyumba za madaktari katika vijiji vya Ormanie na Tinaga.


Mafunzo hayo yamepokelewa vyema na washiriki, ambapo Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Loswash, Bw. Ally Mrisho, alisema mafunzo ya NeST yatasaidia kuhakikisha wanufaika wa TASAF wanapata malipo yao kwa wakati. Bi. Likya Peter, Msimamizi Msaidizi wa Miradi ya TASAF katika kijiji cha Ololosokwan, aliishukuru serikali kwa mfumo huo mpya, akisema utapunguza muda wa kutafuta nukuu za bei za bidhaa kutokana na changamoto za kijiografia za vijiji vyao.


Mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya TASAF, kuhakikisha kuwa wanufaika wanapata haki zao bila changamoto.


Matangazo

  • TANGAZO LA RATIBA YA UCHAGUZI NA UANDIKISHAJI WA UCHAGUZI. September 26, 2024
  • TANGAZO LA UANDIKISHAJI VIJANA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA. October 01, 2024
  • MATOKEO YA USILI WATENDAJI WA KIJIJI.2. September 29, 2024
  • MATOKEO YA USILI WATENDAJI WA KIJIJI. September 29, 2024
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI KUKAMILIKA DARAJA LA JEMA- OLDONYOSAMBU.

    March 09, 2026
  • BARAZA LA HALMASHAURI NGORONGORO LATAMBUA NA KUZIPONGEZA SHULE ZILIZOFANYA VIZURI NA MICHANGO YA WADAU WA ELIMU, KFW, THOMSON Safaris na PWC ZAPONGEZWA. MIL 3.5 ZATOLEWA KAMA ZAWADI.

    February 21, 2026
  • TANAPA, FZS NA KFW WAUNGANISHA NGUVU KUBORESHA MIUNDOMBINU YA KISASA YA SHULE YA MSINGI SOITSAMBU.

    February 18, 2026
  • BARAZA LA WAFANYAKAZI HALMASAHURI YA WILAYA YA NGORONGORO LIMEPITISHA RASIMU YA MPANGO WA BAJETI 2026/2027.

    February 13, 2026
  • Tazama zaidi

Video

Afisa kilimo Ngorongoro aeleza na kufafanua namna ya kupata mazao yenye afya na mbegu bora kutumia katika kilimo.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2026
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2025/2026
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 NGORONGORO
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2023
  • Taarifa na Matangazo
  • Mikataba na Miongozo
  • Taarifa kwa Umma
  • Matokeo ya Upimaji darasa la Nne 2019
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA ELIMU YA KATI NA VYUO VYA UFUNDI JUNE 2019.

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Rais
  • Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2025/-2026
  • NGORONGORO DC YOUTUBE CHANEL

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.